burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Des 2016

Feel Good ya Navy Kenzo yatikisa Israel

Umaarufu wa kundi la Navy Kenzo unazidi kuongezeka kila kukicha. Nahreel na Aika wamenieleza Jumamosi hii kuwa wimbo wao, Feel Good umetokea kuwa maarufu sana nchini Israel.
Wakizungumza kwenye uzinduzi wa video ya wimbo mpya wa Belle 9 aliomshirikisha G-Nako, Give It To Me, Navy Kenzo wamesema DJ maarufu wa Israel, Moshe Buskila aliwatafuta akitaka afanye remix ya wimbo huo.
Nahreel amesema walimtumia sauti tupu na Dj huyo kufanya maajabu kwa kutengeneza remix kali waliyoamua kuijumuisha pia kwenye album yao, Above In A Minute.
DJ Moshe Buskila
Haikushia hapo, Buskila ametayarisha pia wimbo mwingine kwenye album yao uitwao Young. Kwa mujibu wa Nahreel, AIM inaweza kuwa sokoni rasmi December 24.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni