burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Des 2016

Joslin wa Wakali Kwanza arejea na Only You


Unatafuta tafsiri ya swag kwenye nyimbo? Huna haja ya kuchukua kamusi. Ni rahisi sana, sikiliza nyimbo za Joslin. Jamaa huyu ni moja ya rappers ninaowakubali toka kitambo – Perfume, Niite Basi, Nisikilize, verse yake kwenye Dhahabu ya Dully, ngoma za kwenye kundi lake, Wakali Kwanza na zingine kali.
I mean this guy is a hitmaker. Amekuwa kimya kwa muda sasa lakini sasa amerejea, na nathubutu kusema kwa kishindo. Hakuna kitu ninachokipenda kama msanii anapokuwa kimya halafu anarudi akiwa na upya unaompandisha daraja katika uimbaji wake. Kwenye Only You, Jos anadhihirisha kuwa amelisoma vizuri game na kujua sound muafaka ya kuitoa katika kipindi hiki.

Na katika wakati ambao muziki wa Bongo Flava umetengeneza trend ya kile wanachokiita muziki wa biashara kiasi cha kuwafanya wasanii wengi kuimba ladha ambazo zipo nje ya ‘comfort zone’ zao, inafurahisha kumuona Josh akibaki kwenye muziki anaojua zaidi na hivyo kutengeneza kitu chenye upya masikioni.

Ngoma hii inaonesha uwezo wake wa kuswitch kuimba na kurap na vyote katika ubora wa hali ya juu. A great rnb singer, and dope rapper at the same time. Ana switch style comfortably with just a snap of a finger. Huu ni wimbo mzuri si tu kusikiliza kwa melody zake tamu na ujumbe mzuri hususan kwa mrembo wako, bali pia unachezeka kutokana na kuwa beat inayoshawishi kufanya hivyo.
Pia hongera kwa Beef Cha wa MJ Records kwa production hii. Ombi kwa mashabiki wa muziki, nenda Youtube itazame video hii na umuongezee views mkali huyu. Tukipeni support kipaji hiki ili kirejee tena kileleni. Na kwa watangazaji wa redio, wapanga playlist kwenye TV, fanyeni kumrudisha Joslin kwenye chati kwa kuipa airtime kazi yake hii mpya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni