burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Des 2016

Nay wa Mitego afafanua kuhusu ujenzi wa ghorofa yake itayogharimu tsh milioni 300


Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amesema watu wanaoshangaa  na kubisha gharama za ujenzi wa ghorofa yake kufikia  zaidi ya tsh milioni 300 hawajui nini maana ya ujenzi.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nay amedai yeye kwa kuwa anajua nini maana ya ujenzi hivyo hashangai kusikia mtu anajenga nyumba ambayo inagharizu zaidi ya milioni 300.

“Watu ambao wanashangaa nyumba kugharimu zaidi ya milioni 300 sijui niwaweke katika kundi gani,” alisema Nay. “Sema wewe huna pesa ya kufanya vitu kama hivyo lakini unavyokaa  na watu ambao wanajenga nyumba za namna hiyo watakuwa wanakushangaa,”

“Mimi nyumba yangu ya Tabata ikikamilika gharama zote za ujenzi ni zaidi ya milioni hiyo 300. Tena kwa sasa ipo kwenye hatua nzuri, ni hatua ambayo inakula hela hatari kwa watu wa ujenzi wanajua nikiwa na zungumza hivyo ” aliongeza Nay.
Kwa sasa rapa huyo anafanya vizuri na video ya wimbo Sijiwezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni