burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Calisah: Wema Sepetu ni msichana mzuri na mwenye mapenzi ya kweli


Mwanamitindo aliyejipatia jina mwaka huu kutokana na kuwa na uhusiano wa muda mfupi na Wema Sepetu, Calisah, amemwelezea muigizaji na Miss Tanzania huyo wa zamani kuwa ni msichana mzuri na mwenye mapenzi ya kweli.

“Wema ni msichana mzuri, ana upendo, ni mwelewa, ana mapenzi ya kweli, sijaona kasoro kubwa ambayo yeye anayo kubwa tofauti na wasichana wengine,” amesema Calisah. “Ni msichana anayejua kucare, ana real love, pia ana mapungufu yake lakini mazuri ni mengi,” amesisitiza.

Model huyo ameongeza kuwa kwa sasa yeye na Wema hawazungumzi tena baada ya wiki kadhaa zilizopita kusambaa mtandaoni video inayowaonesha wakibusiana kwa mahaba mazito, kitu ambacho kilimkera Wema na kuvunja uhusiano wao.

Hata hivyo Calisah amekiri kuwa uhusiano wake na Wema umemuongezea umaarufu zaidi na kumrahisishia kazi zake.

“Kuwa na Wema imeniongezea kitu nisiwe muongo,” anasema. “Sababu nimekuwa nafahamika mpaka nje ya mipaka ya Tanzania, Kenya, Uganda, kwahiyo imenisaidia. Pia imenirahisia kwenye kazi zangu ninazofanya, hilo namshukuru Mungu japokuwa tumeishia vibaya, umaarufu umekuja wakati mbaya.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni