burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Des 2016

Lady Jay Dee aeleza sababu ya kufanya vizuri kwenye muziki kwa muda mrefu bila kuteterek


Msanii mkongwe wa muziki,  Lady Jay Dee amefunguka kwa kueleza sababu ya kufanya vizuri kwenye muziki wake kwa muda mrefu bila kutetereka.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na remix ya wimbo ‘Together’  akiwa ameshirikiana na mpenzi wake Spicy, amedai siri ya yeye kukaa kwenye game kwa muda mrefu inatokana na kujichanganya kwa kufanya kolabo ya wasanii tofauti tofauti pamoja na kukubali mawazo mapya kutoka kwa watu wake wa karibu.

“Muziki namna ambavyo naufanya mimi kila siku nabadilisha watu wakufanya nao kazi, sifanyi kazi na watu wale wale kila siku pia napokea mawazo kutoka kwa watu wengine tofauti,” alisema Jay Dee. “Kwa sababu naamini kila mtu ana mchango wake awe ni msanii mchanga au mkubwa. Lakini ukisema unafanya kazi na watu wale wale kila siku utakuta muziki wako unafanana, na hiyo ndiyo sababu ambayo inafanya muziki wangu uweze kubadilika kutokana na mazingira,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni