burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

24 Des 2016

‘Hola Hola’ haijaharibu mipango yangu – Chemical


Rapper wa kike Bongo mwenye mistari na swaga za hatari, Chemical amedai kuwa project ya ‘Hola Hola’ haijaharibu mipango yake ya kufanya collabo na rapper mwingine wa kike.

Chemical ameiambia g.lovetz kuwa project hiyo haijaathiri chochote juu ya mipango yake hiyo ila ataangalia kama kuna rapper mzuri atakaye fit kwenye kazi yake atamshirikisha.

“Kukiwa na project yangu yoyote ambayo nitahisi kuna female rapper anatakiwa awepo nitafanya hivyo haimaanishi kuwa Hola Hola ndio imebadilisha mipango yangu wala nini. Lakini kazi yenyewe itabidi tuangalie kama kuna mtu atafiti kwenye kazi yangu nitafanya naye,” amesema Chemical.

Kwa sasa Rapper huyo anafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga kupitia wimbo wake ‘Mary Mary’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni