burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Des 2016

Collabo na msanii wa nje isipofanya vizuri kimataifa ni kazi bure – Fid Q


Rapper Fid Q amesema msanii anapofanya collabo na msanii wa nje na wimbo huo usifanye vizuri kimataifa, ni sawa na kazi bure.

Amesema pia kuwa mafanikio ni pale unapofanya wimbo unaoweza kufika nje wenyewe kama ambavyo nyimbo za nje zinazofanya vizuri hapa nchini.

“Halafu kitu ambacho nawaambia wasanii kila siku, kila mtu anaweza akatengeneza hit lakini lakini tunatengeneza muziki unaoweza ukatrascend?” rapper huyo alisema kwenye mahojiano na mtangazaji wa Uhuru FM, Crispin Mgenge.

“Ninaposema kutrascend namaanisha kwamba ninaweza nikaenda nikawarusha Amsterdam kama ninavyowarusha Mwanza, au tu ninang’aa Mwanza halafu Amsterdam hawanielewi ninafanya nini,” amesisitiza.

“Kwahiyo kutrascend ndio kitu ninachowasisitiza wasanii wajifunze hicho, wasikimbilie tu kufanya ngoma na nani hazisaidii.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni