burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Vitamin Music Group Limited ya Belle 9 yamchukua Gabo Zigamba


Kampuni ya Vitamin Music Group Limited ya msanii wa muziki Belle 9 imemtambulisha mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa EATV 2016, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ kuwa ni msanii aliyechini ya kampuni yao.

Akiongea na waandishi Jumamosi hii mmoja kati ya viongozi wa kampuni hiyo wakati wa utambulisho wa wasanii wa kampuni hiyo katika hafla ya uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ya wimbo ‘Give It To Me’, muigizaji huyo alitambulishwa ramsi kama msanii aliyechini ya kampuni hiyo.

“Kwa sasa ndani ya Vitamin Music Group Limited tupo na Gabo Zigamba, yupo chini yetu kwa sasa,” alisema mmoja kati ya viongozi wa label hiyo wakati wa utambulisho.

Pia Vitamin Music ilimtambulisha Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete kuwa na ni mmoja kati ya viongozi ambao wanashirikiana nao katika kazi zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni