burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Ridhiwani Kikwete afunguka kuhusu bifu zilizopo kwenye muziki

Image result for Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka kuhusu bifu za wasanii zinazoendelea kwenye muziki hapa nchini.

Ridhiwani ameiambia g.lovetz wakati wa uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give It To Me’ Jumamosi hii uliofanyika kwenye beach yake maeneo ya Kawe jijini Dar kuwa wasanii wanatakiwa waache malumbano na waangalie kwenye kujiwezesha zaidi ili waweze kuwa juu kuliko walipokuwa jana.

“Mimi ningewaambia hawa vijana wetu ambao hasa wameanza malumbano kwenye muziki. Tumeshuhudia nchi ikimpoteza mwanamuziki mzuri kama Tupac na Notorious B.I.G kwa sababu ya mambo ya kijinga jinga na yasiyofaa kama haya, wajifunze katika hayo,” alisema Ridhiwani.

“Waache kuangalia nani anafanya nini, waangalie wao wanajiwezeshaje kuwa bora kuliko walivyokuwa jana, watafanikiwa,” ameongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni