burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

21 Des 2016

Joh Makini ataka mfumo wa muziki nchini ubadilishwe

Image result for joh makin
Rapper wa Perfect Combo, Joh Makini amedai kuwa vyombo vya habari wakishirikiana na wasanii wa muziki inabidi wabadilishe mfumo uliopo kwa sasa kwenye muziki.

Joh ameiambia G.lovetz kuwa kwenye tuzo mbalimbali kubwa duniani pamoja na chati za muziki unaweza ukaona msanii mmoja anaingiza nyimbo zaidi ya moja kitu ambacho hapa nchini kimekuwa kigumu kufanyika.

“Nafikiria sisi tukishirikiana na media tukubaliane na huu wakati kwamba sio wakati wa watu kushangaa kwanini msanii mmoja ana nyimbo tatu wenye Top 10 au kwanini msanii mmoja anakuwa kwenye category moja mara tatu. Unajua wenzetu kwenye grammy au nchi zilizoendelea hawashangai hili. Nenda Billboard unaweza ukakuta msanii ana nyimbo tano kwenye Top 10, lakini hapa bongo wanasema nyimbo yake namba moja halafu uingize nyingine? ” amesema Joh.

“Hapana huwezi kuweka nyimbo mbili za msanii mmoja kwenye nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu, ni lazima hayo mambo yaishe. Kama kuna mtu anastahili kuwa na nyimbo tano kwenye chati na ni kali inabidi ziwepo kwa sababu hiyo inawafanya watu wengine waingie studio kufanya kazi nzuri zaidi,” ameongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni