burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Des 2016

Give It To Me ya Belle 9 imeongeza orodha ya ngoma mpya za klabu


Kabla sijazungumzia video na wimbo wa Belle 9, ningependa kumpongeza kwa mwaliko wake wa jana katika uzinduzi wa video hii. Kwa sasa matukio kama hayo ni nadra nchini, lakini ya muhimu sana kwasababu hutoa fursa kwa industry kukutana na kubadilishana mawazo na kuisogeza pamoja zaidi.
Nilifurahi kuwepo pale na hakika ulikuwa ni uzinduzi uliofana. Naupongeza uongozi mzima wa Vitamin Music kwa kufanikisha hili.
Give It To Me bila shaka, inaongeza idadi ya nyimbo zitakazokuwa maarufu kwenye klabu Bongo.

Ninafurahi kuona wasanii wanaanza kuondoa ile imani kuwa Bongo Flava ni muziki wa kusikiliza zaidi, na ndio maana unakuta hafla kama vile harusi au mashindano kama Miss Tanzania, zinajaa playlist za nyimbo za Nigeria.
Huu ni mradi mkubwa wa Belle 9 kwa maana ya uwekezaji alioufanya. Pamoja na kwamba mwaka huu tangu awe na management yake, kazi zake zimekuwa za kiwango zaidi hususan kwenye video, Give It To Me inaongeza nyota moja katika zile alizozikusanya hadi sasa.

Nampongeza pia Belle kumuenzi pia legendary Saida Karoli, na ukweli kuwa ngoma hii imefanywa kabla ya Salome ya Diamond na Muziki ya Darassa na hivyo kufanya uwe mgongano chanya, inaonesha wazi kuwa wasanii wanafikiria zaidi kuweka ‘fusion’ za muziki wa asili kwenye nyimbo zao ili kuzipa ‘Utanzania’ tunaoulilia kila siku.

Wimbo una video nzuri sana na naamini itamfikisha Belle sehemu ambazo bado hajafika. Video imejaa maua (wanawake wazuri) yanayoifanya ivutie sana machoni. Nimependa alivyochangamka kwendana na maudhui na midundo ya ngoma hii na hakuna ubishi kuwa Belle hajawahi miss, yeye huhit tu.
Heko pia kwa G-Nako, kwa nakshi zake kwenye dude hili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni