burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

22 Des 2016

Madaktari wamshauri Darassa kupumzika baada ya kupata maumivu ya kichwa yaliyotokana na ajali

Rapa Darassa baada ya kunusurika kifo katika ajali mbaya ya gari akiwa na muongozaji wa video nchini Hanscana huko Kahama, Jamatano hii alienda katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwaajili ya kucheki afya yake.
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii akiwa hospitalini hapo, Darassa alisema aliamua kwenda kucheki afya yake baada ya kuwa na maumivu ya kichwa yaliyotokana na ajali hiyo.

“Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana,” alisema Darassa.

“Wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na kutibu hayo maumivu ya kichwa,”
Darassa na Hanscana pamoja na wenzao wawili alipata ajali hiyo wakati wakiwa njiani wakitokea Kahama mkoani Shinyanga kwenda Kakola mkoani humo kwaajili ya show.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni