burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Apr 2017

Antonio Conte wa Chelsea amekiri kikosi chake kimekutana na magumu.


Meneja wa klabu ya Chelsea,Antonio Conte, amekiri michezo miwili waliocheza siku za hivi karibuni yamekua michezo migumu kwa upande wao na imekua muhimu kuhakikisha wanapata alama tatu zitakazowasaidia kujikuta kileleni mwa ligi hiyo ya Epl.

Conte ambaye ni raia wa Italia, amewasifia wachezaji wake kwa kupambana hadi kuhakikisha wanachomoza na ushindi huo Mnono wa magoli 4 kwa 2 mbele ya kikosi cha Southampton, na anaamini kuwa wachezaji wake watapambana na kuhakikisha wana nyakua Ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwa Msimu huu.

Meneja huyo mwenye Mizuka pindi timu yake inapopata ushindi, amesema kuwa anahitaji kukipumzisha kikosi chake baada ya Michezo hiyo migumu waliokutana nayo wiki hii.

Aliyekuwa Mwiba katika mchezo huo uliopigwa hapo jana ni nyota wa timu, Eden Hazard aliyeanza kuiandikia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 5 ya mchezo. Katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, beki Gary Cahill alifunga bao la pili.

Katika kipindi cha pili mshambuliaji mahiri wa Chelsea, Diego Costa aliongeza mabao mawili, huku mabao ya Southampton yalifungwa na kiungo Oriol Romeu na beki Ryan Bertrand.

The Blues wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 78 wakiwa wamecheza michezo 33 huku Tottenham ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama 71 wakiwa nyuma ya Chelsea kwa mchezo mmoja.


Majogoo wa London, klabu ya Liverpool, inashikilia nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 66 huku matajiri wa Uingereza Manchester City, wakishikilia nafasi ya 4 wakiwa na alama zao 64 nyuma ya klanbu ya Mashetani wekundu Manchester United inayoshikilia nafasi ya 5 na alama zao 63 wakiwa nyuma kwa alama 1 dhidi ya City.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni