burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Wenger hapata kigugumizi kuzungumzia hatma yake ndani ya Arsenal


Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, anasema kuwa hatma yake ya baadaye “haitawatatiza kwa vyovyote wachezaji.”

Aidha, Wenger anakiri kuwa mabao 3-0 waliofungwa na timu ya Crystal Palace ni “jambo la kuleta wasiwasi mkubwa”.

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu, huku akikabidhiwa mkataba mpya wa miaka mingine miwili, ingawa hajatangaza iwapo ataendelea kuifunza Arsenal au la.

Arsenal ambayo ipo katika nafasi ya 6, iko na alama saba nyuma ya timu nne zilizoko katika nafasi za kwanza, huku ikisalia na mechi nane tu kukamilisha msimu huu.

“Nimeiongoza Arsenal katika mechi 1,100, na hatujawahi kushindwa namna hii,” amesema mfaransa huyo.

“Ilibidi tujibu mara moja, lakini hatujakubali.”

Hii inawaacha katika hatari kubwa ya kukosa kufikia timu nne bora zitakazomaliza msimu huu, kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 67 iliyopita.

“Naelewa namna mashabiki wetu waIivyokata tamaa, nasi pia tumetamaushwa mno,” alisema.

“Ni jambo la kutia wasiwasi na kukatisha tamaa, jinsi tulivyopoteza mechi hii. Wachezaji wa Crystal Palace walikuwa wakakamavu, waliicharaza Chelsea hivi majuzi, na hiyo inaonesha bayana kuwa ni wachezaji bora.

“Tuko katika hali mbaya. Mechi hii haijasaidia chochote.” Alisema Arsene Wenger

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni