burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Bill Nass afafanua nyimbo zake kutumiwa kama vijembe na watu kwa wenzao


Bill Nass amefunguka sababu ya nyimbo zake kutumiwa na watu kama vijembe kwa wenzao.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, kinachoendeshwa na Nico Track, kuwa nyimbo anazoziimba yeye zinatokana na matukio ambayo yanatokea zaidi mitaani ndio maana inakuwa rahisi zaidi kutumiwa na watu wengine ikiwemo hata kuandika ujumbe wa nyimbo zake sehemu mbalimbali.

“Mara nyingi huwa naandika vitu ambavyo vinarelate na vitu vingine, nilivyimba ‘Ligi Ndogo’ kuna watu walisema nimewaimbia watu wengine. Nilivyosema ‘Sitaki Mazoea’ ndio nafsi nyingi hazitaki mazoea kwa sababu mazoea ndio yanakuja kuharibia watu CV na kujuana sana ndio kuleta matatizo,” amesema.

“Hakuna mtu anayependa mazoea kuzidi na mtu yoyote akikuzoea kuzidi anakudharau au heshima yake haitabaki pale ilipokuwa awali lakini niliimba kwa hisia za watu wengine lakini kuwakilisha kile ambacho mimi ninakiamini. Nyimbo zote nazozifanya huwa naanza na mimi kwanza kama mwananchi wa hali ya chini, kama mtanzania au kama mtoto wa kiume,” ameongeza.

“Nyimbo kama hiyo haiwezi kufa ndio maana unakutana na daladala limeandikwa Ligi Ndogo, Chafu Pozi au unakutana na bajaji imeandikwa Hatutaki Mazoea kwa sababu ni vitu ambavyo vip mitaani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni