burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Apr 2017

Harmonize: Kumuona Diamond akizidi kupambana kunanipa nguvu


Kati ya waimbaji kutoka Bongo waliokubalika Kenya ndani ya muda mfupi ni pamoja na Harmonize. First born huyo wa WCB alitesa speaker zetu na wimbo wake, Aiyola ambao ndio ulimtambulisha rasmi kama msanii kanda hii.

Baada ya hapo, Harmonize aliendelea kuachia hit baada ya hit, na wimbo ‘Bado’ aliomshirikisha bosi wake hatousahau kamwe, kwani ndio wimbo uliomnyanyua na kufanya ukubwa wa jina lake kuongezeka. Leo hii yupo miongoni mwa wasanii wakubwa sio tu Tanzania.

Wiki hii, msanii huyo anayemiliki tuzo ya Afrimma amezuru Kenya na kama desturi, Mzazi Willy Tuva alimkalisha Msetoni wakapiga story na kuongelea mawili matatu.Kwenye mahojiano, alimtaja bosi wake kama sababu ya yeye kuzidi kujitahidi katika safari yake ya muziki.

“Sasa hivi Diamond ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa Tanzania, lakini bado anapambana. Tunavyoongea Diamond yupo South Africa kwa ajili ya kazi,” alisema.

“Kama Diamond ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa Tanzania na hana time ya kurelax, hiyo inanipa nguvu kuzidi kupambana na mimi,” aliongeza Harmonize.

Katika hatua nyingine, aliwataka mashabiki wake kuweka macho kodo kwenye tovuti yao ya Wasafi.com kwa ajili ya kitu kipya kitakachodondoka exclusively wakati wowote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni