burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Drogba amejiunga na hii timu kama mchezaji na mmiliki nchini Marekani


Mcheza soka wa kimataifa wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast, ambaye amewahi kuichezea Chelsea ya Uingereza Didier Drogba amerudi tena kwenye soka kwa mara ya kwanza toka aachane na timu ya Montreal Impact.

Drogba ambaye kwasasa ana umri wa miaka 39 aliachana na timu ya Montreal Impact kwa miezi kadhaa na kukaa bila timu licha ya kuwa alipokea ofa nyingi kutoka katika timu mbali mbali za England, China, Ufaransa na timu ya Corinthians ya Brazil baada ya kuichezea Montreal kwa miezi 18.

Drogba ametangazwa kujiunga na timu ya Phoenix Rising FC ya Marekani iliyopo daraja la tatu (American’s United Soccer League) akiwa kama mchezaji na sehemu ya mmiliki wa timu hiyo.

Drogba ambaye ana malengo ya kuiwezesha Phoenix ishiriki Ligi Kuu Marekani (MLS) mkataba wa kuichezea timu hiyo unaweza kuwa wa misimu miwili au mitatu na pia atakuwa ananafasi ya kuamua kama kuwa kocha au sehemu ya utawala wa timu hiyo, Drogba ana hisa katika timu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni