burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

15 Apr 2017

Roma awa gumzo mtandaoni kwa kitendo cha kuimba wimbo wa kumsifu Mungu kuhusu kilichomkuta


Msanii wa muziki wa hip hop Roma Mkatoliki Ijumaa hii katika mitandaoni ya kijamii amekuwa gumzo baada ya kuonekana akiimba wimbo wa kumsifu Mungu ikiwa na wiki moja toka atekwe na kuachiwa.

Katika video hiyo rapa huyo amelalamika jinsi watu wanavyomsema vibaya kutokana na matatizo hayo ambayo yalimkuta akiwa na wenzake watatu.

Roma alisisika akisema “Ninalalaa macho wazi mimi, kama ndege mkiwa juu ya paaa, Nimekuwa kama muhuni mimi, fanya ima, fanya ima bwana uniokoee. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu mimii bwanaa, kila nipitapo kunisema nakunicheka, munguu wangu mbona umeniachaa,”

Rapa huyo na wezake walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa Tongwe Record na baadaye kutelekezwa katika beach za Uninio Jijini Dar es salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni