burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Apr 2017

MANCHESTER UNITED YASHIKWA SHATI NA ANDERLECHT


Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Anderlecht katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Europa Ligi uliochezwa hapo jana Usiku huko Constant Vanden Stock Stadium jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Henrikh Mkhitaryan alianza kuifungia bao la kuongoza Manchester United katika dakika ya 36 ya mchezo kwa mkwaju wa karibu lakini katika dakika ya 86 ya mchezo makosa ya mlinzi Matteo
Darmian yalitoa nafasi kwa Leander Dendoncker kuifungia Anderlecht bao la kusawazisha kwa kichwa na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Timu hizo zitarudiana tena Aprili 20 mwaka huu huko Old Trafford jijini Manchester.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni