burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

19 Apr 2017

Hanscana alia na copy & paste za waongozaji wa video za Bongo


Hanscana ambaye ni mmoja kati ya waongozaji wa video za muziki nchini ambao wanafanya vizuri, amelaani kitendo cha baadhi ya waongozaji wa video ambao wana-copy idea za nje na kuzileta ndani.

Muongozaji huyo amedai kutegemea kukopi vitu vya kutoka nje ya Bongo kama vile nchi za Afrika kusini ni kuua ajira za watu wengi wa Afrika Mashariki.

Hascana kupitia ukurasa wake Instagram amefungukia hayo akiwa ameweka picha yake na msanii Eddy Kenzo kutoka Uganda na kudai kukopi kazi za watu wa Magharibi na Kusini ni kupoteza utambulisho wa sanaa ya Afrika Mashariki hivyo kutoa ahadi ya kupigania.

“Nitahakikisha game ya Afrika Mashariki inafika mbali zaidi kupitia muziki wetu wenyewe pamoja na video zinazozalishwa hapa hapa nyumbani Afrika Mashariki na waandaji wa hapa hapa E.A, Ili sanaa yetu izidi kujitosheleza ( kujitegemea zaidi ) na siyo mpaka tukakopi vitu toka Kusini ya mbali ama umagharibi na kupelekea kupoteza ‘Id’ yetu kisanaa na mbaya zaidi kuua ajira za vijana lukuki wanaotegemea sanaa hii dancers, models, make up artist, designers, producers ETC nina amini sana katika sisi”- Hanscana aliandika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni