burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Apr 2017

Sijui chochote kuhusu kuibiwa kwa nyimbo ya ‘Show Me’ – Ray C

Image result for RAY C
Wiki iliyopita, kuliibuka mazito kuhusu wimbo wa Harmonize ft Rich Mavko uitwao ‘Show Me’. Wimbo huo unadaiwa kuibiwa kutoka kwa msanii PCK anayeishi Uingereza, huku Ray C akitajwa kama shahidi namba moja, kwa kuwa alikuwepo studio wakati msanii huyo chipukizi anarekodi.

Baada ya kupata maneno kutoka kwa Hamonize na mtayarishaji wa ngoma hiyo kutoka Wasafi Records, Laizer, sasa G.LOVETZ imefanikiwa kuongea na Ray C kuhus sakata hilo.

Ray C amegoma kuongelea lolote kuhusu hicho kinachoendelea kwa kusema, “Aisee siwezi kuongea hizo vitu hazinihusu mimi, simjui.”

Katika mahojiano tuliyofanya na Harmonize alikataa kuzungumzia hilo kwa madai kuwa mambo hayo tayari yapo chini ya uongozi wao wa WCB, lakini Laizer alidai kuwa hamfahamu msanii huyo na wala hajawahi kusikia jina kama hilo na kuongeza kuwa, kama aliwahi kurekodi katika studio zao basi lazima atakuwa amepewa risiti kwa hiyo anaweza kuionyesha kama ni kweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni