burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Apr 2017

Simba wapewa Pointi 3 na kamati ya masaa 72


Klabu ya Simba imepewa Pointi 3 na magoli matatu baada ya kikao cha kamati ya Saa 72 kuthibitisha kuwa mchezaji Fakhi Mohammed wa Kagera Sugar alikuwa na kadi tatu za njano katika mchezo dhidi ya Simba April 2,2017,uliopigwa Kaitaba

“Mchezaji huyu alipata kadi ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Mbeya City, akapata kadi nyingine ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Maji Maji na pia alipata kadi ya njano kati ya mchezo wa Kagera Sugar na timu ya African Lyons,” alisema Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Yahaya.

Faki alicheza kwenye mchezo wa Kagera Sugar na Simba uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba ambapo timu yake ilimzamisha Mnyama kwa mabao 2-1.

Sasa Simba wapo kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara wakiwa na Pointi 61 huku Yanga wakishika nafasi ya pili wakiwana Pointi 56

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni