burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Barakah The Prince awawakia mashabiki ishu ya picha yake na Babu Tale ‘wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha?’

Msanii wa muziki Barkah The Prince amewaonya mashabiki wasimpangie maisha binafsi na kwamba wao kinachowahusu kutoka kwake ni muziki mzuri tu.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Acha Niende’ ametoa kauli hiyo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii anayetafsiriwa kuwa ni hasimu wa msanii mwenzake kutoka katika lebo yao ya Rock Star 4000.

“Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Katika hatua nyingine Baraka ameweka wazi kuwa tangu kusajiliwa katika lebo ya Rock Star chini ya Bi. Seven Mosha kumemuongezea nafasi na wigo mpana wa kujulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani kubwa katika maisha yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni