burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Chris Brown alia na mpenzi wa Karrueche Tran, Quavo


Chris Brown ana hasira na Quavo wa kundi la Migos.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kuwa na mahusiano na Karrueche Tran amemuita Quavo ni msaliti kutokana na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo wake huyo wa zamani.

Chanzo cha ndani kimeuambia mtandao wa TMZ, Brown ameumizwa na kitendo alichofanya member wa kundi hilo la Migos ambao alikuwa na ukaribu nao zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya nao kazi kwa kushirikishwa katika wimbo wao ‘Just For Tonight’.

Wakati huo huo Chris alidhihirisha ukaribu zaidi na wasanii hao baada ya kuipa nguvu albamu yao ya ‘Culture’ kwa kusaidia kuipromoti. Hitmaker huyo wa Party, anaamini ukaribu wa Karrueche na Quavo ulitokea baada ya yeye kuwa na urafiki na kundi hilo.

Brown aliwahi kufanyiwa mahojiano na Billboard kuhusu kundi la Migos, alisema, “my real friends and brothers” and said, “I will never hate on you ni**as.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni