burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Matokeo ya mechi za robo fainali za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa April 12, 2017


Mchezaji Cristiano Ronaldo hatimaye amemaliza ukame wa miezi saba kwenye ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo ambao Bayern Munich wamepoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Real Madrid.

Kwa sasa Ronaldo amefikisha magoli 100 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji Ulaya.

Kiungo Arturo Vidal alipachika goli la kwanza lakini akakosa nafasi ya kuandika goli la pili baada ya kupaisha mkwaju wa penalti alioupiga.

Javi Martinez alipatiwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.

Bayern walitawaliwa baada ya kadi nyekundu na kujikuta muda mwingi wakiwa wanatafuta mpira.

Haya ni matokeo ya mechi zingine za kwanza za robo fainali za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa April 11 na April 12 2017.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni