burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Apr 2017

Uwe Wangu ya MB Dog ina umri wa mtoto wa darasa la kwanza


MB Dog amefunguka kuwa wimbo wake mpya ‘Uwe Wangu’ una umri wa mtoto wa kukaribia kuanza darasa la kwanza.

Muimbaji huyo amedai kuwa wimbo huo una miaka takribani sita tangu alipouandika lakini hakuweza kuutoa kwa kipindi hicho ndipo alipoamua kuutoa mwezi uliopita kama bonus track kwa mashabiki wake.

Akiongea na mtangazaji wa Abood FM katika kipindi cha Mega Mix, Simple Bway, Dog amesema, “Hii ngoma haikuwa official ilikuwa ni bonus track. Ni miongoni kwa nyimbo nilizozifanya kidogo miaka ya nyumba, hii ngoma ina miaka kama sita hivi nyuma tangu niingize sauti, ni umri wa mtoto mdogo anakuwa kabisa anatembea na anaongea vizuri.”

Ameongeza, “Kwa sababu ipo na ramani tulikuwa hatujaseti za kuachia mdundo ambao upo kwenye plan nikafikiria na wakati pia umeenda nikaona bora niwape watu tu ili wajue Dog yupo na nisipotee sana,” ameongeza.

Msanii huyo amesisitiza kuwa hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya uitwao ‘Ashashi’ ambao umetayarishwa na Man Walter.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni