burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Apr 2017

MADEE AMASIFIA NAY WA MITEGO


Msanii na hitmaker wa ngoma Hela ‘Madee Seneda’ azungumzia hali ya kinachoendelea kuhusu mzuki wa Tanzania, wasanii na  serikali.

Akizunumza na G.LOVETZ Made amezungumzia tukio lililomkuta Nay wa Mitego na kusema kuwa kinachofurahisha zaidi kwamna inaonekana kabisa serikali inasikiliza nyimbo za wasanii hivyo kikubwa wasanii wawe makini katika kufanya kazi zenye tija na lengo jema kwa mashabiki na serikali yao.

“hii inaonesha kabisa kwamba serikali inasikiliza muziki wetu kwa ukaribu unajua mwanzo watu walikuwa wanaogopa kuandika vitu kama anavyoviandika Nay lakini kwa mabacho amekifanya nadhani amewafungua pia wale wengine ambao wana system ya kuandika ngoma kama zile…lakini kwa kitu ambacho kimetokea kuruhusu ile nyimbo ya Nay iendelee kusikilizwa na ni neema kubwa sana kwenye muziki wa bongo fleva na ninampongeza Nay” Alisema Madee.

Hata hivyo Madee ameongeza kusema kuwa hana haraka na mfumo wa kile kinachoendelea katika kuachia wimbo na ataendelea na umfumo wake wa kuachia ngoma moja kwa mwaka ili aweze kuwaachia nafasi wasanii wengine wapate nafasi ya kufanya wanachoweza kwenye muziki wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni